Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

MAWAZO HUBADILI MAISHA

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Majengo, biashara kubwa, viwanja vizuri vya mpira na mengine mengi ambayo wengine huita maajabu ya dunia ni matokeo ya mawazo. Ninachotaka kusema ni kwamba kila mtu ana mafazo ambayo akiyafanyia kazi maisha hayatakuwa kama yalivyo sasa. Mtihani mkubwa ni jinsi ya kuyapata mawazo yako ambayo yako ndani yako mithili ya madini. Wote tunatambua madini si rahisi kuyapata ni mpaka nguvu ya ziada itumike maana hukaa chini sana na mengi ya madidini kama sio yote yako chini ya miamba. Watu hulazimika kununua mitambo ili tu waweze kufikia madini. Kifupi si lelemama. Vivyo hivyo kwa mwanadamu ili kukutana na mawazo kuntu yaliyomo ndani yake, ni lazima afanye kazi ya ziada. Yawezekana umejaribu mawazo mengi kufanyia kazi lakini mambo bado hayajabadilika. Hii haimaanishi ya kuwa wewe huna m...

UMEFANYA NINI KATIKA MAISHA YAKO?

Wazo La Leo: Habari ya   leo rafiki na msomaji wa mtiririko wa Makala za kila siku zijulikanazo kama wazo la leo. Leo nataka niongelee kidogo juu ya: Umefanya nini katika maisha yako? Swali laweza mfikirisha sana mtu, lakini kifupi toka uzaliwe umefanya nini ili hata uweze sema angalau nimefanya jambo/kitu ambacho ninaweza sema hakika sijutii kuzaliwa kwangu. Wengi ni tatizo maana hadi muda huu ujumbe huu unawafanya wajishangae maana wakiangalia nyuma hawaoni kabisa kitu/jambo lenye tija ambalo limefanyika. Leo hebu nianze kukuambia rafiki yangu, Sehemu ya kwanza ambayo imesababisha tushindwe kufanya mambo yenye maana ni kule kusjishughulisha na shughuli tusizo zipenda. Umewahi sikia watu wakishangilia siku ya Ijumaa inapofika. Wengi utasikia asante Mungu ni Ijumaa leo. Usemi huu hubeba ujumbe mkubwa sana ya kwamba sasa nakwenda kuisahau hii shughuli na kupumzika. Watu wa jinsi hii wako lukuki. Ukisikia maneno yatokayo vinywani mwao ni kulaani viongozi, kulaani utaratib...

UPINZANI ULIOPO KATI YA UBONGO NA MOYO

Wazo La Leo Habari ya   leo rafiki na msomaji wa mtiririko wa Makala za kila siku zijulikanazo kama wazo la leo. Leo nataka niongelee kidogo juu ya upinzani uliopo kati ya ubongo  na moyo. Ninapoanza kuelezea naomba nikuulize kitu kitogo: Je unajua kwa uhakika wewe una kitu kisicho cha kawaida ndani yako kiwezacho kubadili kabisa maisha yako na mengine yakawa stori? Kama hujui naomba nikuambie ya kwamba maisha unayoishi sasa mfanano wake ni tone ndani ya bahari.  Huna haja ya kuwa tone kwani wewe ni bahari. Sababu moja kubwa inayokufanya ushindwe kuishi kwa viwango vya juu ambapo ni haki yako ni ukinzani uliopo kati ya moyo na ubongo. Unaweza kuona jambo linafanywa na mtu na ukajisemea  moyoni ya kuwa nami naweza kufanya lile afanyalo yule (MOYO). Ghafla unaanza kujiongelesha hivi nitawezaje (UBONGO)? Yaani unaanza angalia uwezakano wa wewe kufanya na ukiendelea kutafakari unajiambia siwezi. Sasa ubongo       umesema huwezi lakini na unakuu...

NGUVU NA MUDA WAKO UNAUWEKEZA WAPI?

Wazo La Leo Karibu tena msomaji wa Makala Naamini umewahi kujiuliza na kama bado basi endelea kufuatana nami juu ya  mada yetu ya leo isemayo Nguvu na muda unauwekeza wapi? Kimsingi kila mmoja wetu kwa namna moja au nyingine kuna mahali anawekeza muda na nguvu zake. Nini namaanisha nini nisemapo kuwekeza muda na nguvu? Kimsingi chochote ufanyacho lazima utumie muda na nguvu pia. Hii ndio naita kuwekeza. Hebu niachane na sehemu ambayo wewe huwekeza muda na nguvu zako, nami nijikite kwenye uwekezaji wenye tija. Kujiendeleza Kama kuna kitu ambacho mwanadamu amefumbwa basi ni eneo la kujiendeleza (Pesornal Development). Hivi umewahi kujiuliza ni kwa nini umekuwa hupigi hatua? Au kwa nini umekuwa mtu wa uhitaji kila mara na kuzungukwa na madeni mpaka umegeuka kituko utazani unafanya maagizo barabarani maana  kwa jinsi ugeukavyo mara umuonapo mdeni wako Joti atasubiri sana. Wewe tunayekuona siye wewe. Wewe mwenyewe yuko ndani yako. Maana yake mko wawili wewe wan ...

Siri ya Maisha ni nini?

Siri ya mafanikio inaishi wapi? Wewe unajitambua? Muda wako wa kujiweka huru umefika. Ninakuweka huru kuanzia sasa. Je, uko tayari? Anza na maswali haya: 1) Huwa unalisha tumbo lako kila siku? 2) Huwa unalisha ubongo wako kila siku? 3) Huwa unalisha moyo wako kila siku? Ninakuweka huru kwa kukulipa sarafu yenye pande tatu kwa majina yake ni: #1. Jana yako #2. Kesho yako #3. Sasa yako Mwendo wa jaribio (experiment) Kwanza. Leo ni leo. Anza kutembea kuelekea kwenye mafanikio yako. Unaijua njia? Anza kutembea kwa miguu yako miwili. Kama huna miguu na uanze kufanya kile unachoweza utoke hapo ulipo hadi sehemu nyingine. Tembea kama vile maisha yako yote yanategemeana na kutembea huko. Kiuhalisia kutembea kwako ndo muujiza wa kujiweka huru. Unashangaa? Ni hivi: Miili yetu inashibishwa sumu kibao kwa hewa tunayopumua na vyakula tunavyokula. Hewa ina Carbon dioxide kutoka kwenye moshi wa magari (pollution) na viwanda. Vyakula vina dawa za mimea(pesticides). Itapendeza k...

Unaulisha nini mwili wako?

Unakula chipsi na soda kila siku? Umeacha kula mboga za majani? Tabia zako zikoje linapokuja suala la lishe? Acha kula Msosi usio na virutubisho. Unaulisha nini ubongo wako? Hili ndo suala nyeti kuliko lishe. Acha kusoma magazeti ya udaku! Acha kutumia Dopamine zako vibaya. Unaweza kusema wajinga wapumbavu huliwa na wajinga werevu. Ukiangalia magazeti ya udaku yakishapambwa na picha na vichwa vya habari vya mambo ya udaku, basi kila mtu atakimbilia kulinunua. Cha kufurahisha zaidi mara nyingi tunachoambulia ni kuangalia picha na umbeya usio na maana yoyote. Hata msomaji haongezeki thamani hata kidogo. Tunatumia muda mwingi kusoma magazeti kwa sababu tunataka kujuzwa mambo. Je, ni lazima tujizwe kila aina ya uchafu kama dodoki? Ni lazima tuwe zoa zoa kama dodoki? Tunapojuzwa vitu visivyo na maana ni kwa faida ya nani? Huo muda tunaopoteza nani anatulipa? Vitu vingi vinavyoandikwa kwenye magazeti ya udaku havidumu. Ukizingatia jinsi ambavyo teknologia imerahisisha mawasil...

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...