Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 22 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza juu ya AINA 5 ZA UFAHAMU ULIOTIWA SUMU JUU YA UWEKEZAJI. Makala iliyopita tuliongelea na kumalizia aina ya nne ya sumu juu ya uwekezaji. Leo naanza kuongelea aina ya tano na nikuombe endelea kunifuatilia:- . 5. Utajiri/Dhana ya mali/vitu kuwa ndio utajiri Kama unadhani ukijilimbikizia mali ndio utajiri naomba nikupe pole kwani hiyo pekee ni ubinafsi na utakutesa sana. Ninapoongelea mafanikio namaanisha kuacha alama, kugusa maisha ya watu wengine. Huwezi kujiita umefanikiwa kama huna mawazo ya kugusa jamii kwa mahitaji mbalimbali. Huu ndio utajiri wa kweli kufanyika baraka kwa watu wengine. Siri kubwa ya kufanikiwa ni kuelewa kwa kina dhana ya uwekezaji – Hapa msisitizo ni kwamba unawaza chochote upatacho utawezaje kukizidisha na wala si kupanga matumizi. Napenda hapa twende p...