Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 15 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza juu ya Laana. Kama ambavyo tumejifunza katika Makala zilizotangulia, umasikini ni roho na pia laana. Hakuna jinsi ya kukwepa kuuelezea umasikini pasipo kuhusisha nyanja ya roho. Ninachotaka ukijue pasi shaka ni kwamba baadhi ya umasikini ni kutokana na laana. ‘Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata. Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani. Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia. Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo, Bwana atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangam...