Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 26 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza juu ya kwa nini uko jinsi ulivyo. Kwa nini uko njinsi ulivyo – Kuna mambo unatakiwa kuyajua ambayo yanachangia sana kukutengeneza na kuonekana jinsi ulivyo. Leo tunakwenda kuangalia jambo la tatu linalomtengeneza mtu:- UMEZUNGUKA NCHI YAKO/DUNIA KWA KIWANGO GANI? – Kitendo cha kuzalia, kukulia, kusoma na kisha maisha katika nchi yako bila kuona sehemu nyingine ya dunia ikoje kumembupaza wengi na mbaya zaidi wengine wamezaliwa kijiji X wamesoma kijiji X wameoa kiji X na maisha yote hadi kuzeeka na kufa wangali kijiji X. Niambie mtu wa jinsi hiyo atakuwaje kuchukulia mambo maana ayajuayo ni ndani ya mipaka yake na wala hajui upande mwinge wa dunia mambo yakoje. Watu wa jinsi hii wameishia na maisha yasiyoridhisha na kuwa na mtazamo usiozidi mipaka yao. Mithali 4:7 Bora hekima, basi jipatie heki...