Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2018

Utaambulia nini kwenye Wazo la Leo?

Utaambulia nini kwenye Wazo la Leo? Jifunze kutambua vitu muhimu kwenye maisha yako kwanza. Vingine ni vya ziada. Hiyo yaweza kuwa siri ya maisha bora hapa Duniani. Kupokea na Kutoa ni kama watoto mapacha. Siku zote wanaongozana pamoja haswa wanapokuwa wadogo. Leo hii tunaishi kwenye Dunia yenye fursa mbalimbali. Fursa hizo zinatubariki na pia tunazitumia kubadili wengine. Ni sawa na kusema tunapokea na pia kutoa. Haijalishi ni fursa gani iko mbele yako, kama ni kusoma, kazi, kupata mwenza au hata kitu chochote ukipendacho kinachokupatia maarifa kama vile Karakana ya Ubongo, hizo zote ni fursa. Madhalani tunapenda kuishi. Tufikirie pamoja maswali ya kujiuliza ili tufanye majaribio (Experiments). Tusipende sana kukimbilia majibu maana ni njia rahisi zaidi ya kujiua. Haswa jibu linapokuwa siyo lenyewe . Ni vizuri kutambua ya kuwa, hata unapokuwa umeshapata jibu la kwanza, endelea kufikiri ili upate jibu la pili, tatu, nne na kuendelea ili usiwe Mfu. Ipe akili isiyoonekana kazi ya ...

Namna ya kutengeneza na Kuishi maisha Bora

Utaambulia nini kwenye Wazo la Leo? Jifunze kutambua vitu muhimu kwenye maisha yako kwanza. Vingine ni vya ziada. Hiyo yaweza kuwa siri ya maisha bora hapa Duniani. Kupokea na Kutoa ni kama watoto mapacha. Siku zote wanaongozana pamoja haswa wanapokuwa wadogo. Leo hii tunaishi kwenye Dunia yenye fursa mbalimbali. Fursa hizo zinatubariki na pia tunazitumia kubadili wengine. Ni sawa na kusema tunapokea na pia kutoa. Haijalishi ni fursa gani iko mbele yako, kama ni kusoma, kazi, kupata mwenza au hata kitu chochote ukipendacho kinachokupatia maarifa kama vile Karakana ya Ubongo, hizo zote ni fursa. Madhalani tunapenda kuishi. Tufikirie pamoja maswali ya kujiuliza ili tufanye majaribio (Experiments). Tusipende sana kukimbilia majibu maana ni njia rahisi zaidi ya kujiua. Haswa jibu linapokuwa siyo lenyewe . Ni vizuri kutambua ya kuwa, hata unapokuwa umeshapata jibu la kwanza, endelea kufikiri ili upate jibu la pili, tatu, nne na kuendelea ili usiwe Mfu. Ipe akili isiyoonekana kazi ya ...

Mazingaombwe ya Kukopi na Kupesti

Mazingaombwe ya Kukopi na Kupesti Yanahitaji Ufanye Uchunguzi (Experiment). Wewe uko wapi sasa? Uko ndani ya Gari ipi? Mdogo mdogo Gari ya Karakana ya Ubongo inasogea. Hatuhitaji kujiongezea dopamine iliyo nje ya mwili ili upate stimu ya kusonga mbele. Inawezekana kuwa mjanja bila dopamine ya vitu kama kulewa na madawa ya kulevya. Watu wengi wenye magonjwa mbali mbali yanayosumbua sana wanahitaji kuacha kujiongezea dopamine kienyeji. Tusipobadilika sisi wenyewe hakuna kitu chochote nje yetu kitakachodubadilisa. Hata ujiongezee dopamine kiasi gani. Ni suala la kujijengea tabia stahiki kama vile kwenda kitandani kulala ukiwa vizuri zaidi ya jana yako (Go to bed smarter than yesterday). Mwandishi maarufu wa Tanzania ambaye ameandika kitabu cha Kusudia Kuwa Wewe, Bwana Lameck A. Hulilo huwa anapendelea kusema: ‘Inawezekana. Hebu jitafutie hicho kitabu uone jinsi unavyoweza kufanya mazingaombwe ya kuwa ulivyokusudiwa kuwa bila ku-kopi na ku-pasti walivyo wengine. Bila kutumia...

Mazingaombwe ya Bahari Mbili

Mazingaombwe ya Bahari Mbili: Wanakarakana ya Ubongo! Mwaka ni mpya bado. Leo ninaongelea mazingaombwe yanayotokea kwenye mazingira yanayotuzunguka. Kuna Bahari mbili humu Duniani ambazo maji yake yanatokea Mto Jordan. Bahari ya kwanza inaitwa "Dead Sea" kwa lugha ya wenzetu. Au Bahari Mfu kwa lugha yetu. Hii Bahari Mfu japo ni Bahari lakini imekaa kama Ziwa. Inasemekana kwamba maji yake yana chumvi nyingi sana kiasi kwamba hakuna kiumbe chochote kile kinachoweza kuishi kwenye maji hayo. Hakuna cha Samaki wala Mamba wala Nyangumi, wala uhai mwingine wowote kama vile mimea ya Baharini vinavyoweza kustahimili hicho kiasi cha chumvi ya maji ya Bahari Mfu. Na ndo uhalisia wa hilo jina lake. Wataalamu wanatuambia chumvi iliyomo ndani ya Bahari Mfu ni nyingi kiasi kwamba hata mwili wa binadamu unaelea kwa urahisi kabisa. Kiwango cha hiyo chumvi ni mara kumi zaidi ya viwango vya chumvi vilivyomo kwenye maji ya Bahari nyingine unazozijua wewe. Bahari nyingine inaitwa Galilee. ...

Mazingaombwe ni sehemu ya Maisha! Chagua yale yenye Manufaa kwako.

Wana Karakana ya Ubongo! Jana niliongelea jambo moja kuhusu namna ya kusoma akili za watu kwa kutumia kitu nilichokiita mazingaombwe. Kuna siri kubwa ndani ya kufanya mazingaombwe. Pia unahitaji ujuzi wa hali ya juu. Kwa maana hiyo wale wanaoifanya kazi hiyo hutumia muda mwingi sana kujifunza. Huwezi kukurupuka na kujua siri hizo kwa siku moja. Siku hizi kuna Talk za Shows ambazo zinaonyesha siri za matukio mbalimbali ya mazingaombwe. Hata watoto kwenye baadhi ya mashule wanafundishwa mbinu ndogo ndogo kwa njia ya Hesabu, sarafu na karata. Mfano wanafundishwa namna ya kufanya sarafu itokomee kusikojulikana na pia ikaonekanie mahali pengine. Ni aina ya burudani kama hujui siri ya kinachofanyika. Pia wanatumia karata kusoma ubongo wa mtu kumwambia karata aliyofikiria kwenye akili yake. Kuna wakati kama mtu sio mzoefu anaweza kukosea. Kwa hiyo unatakiwa umakini mkubwa. Kwenye moja ya Talk shows, kuna mwana mazingaombwe mmoja ambaye anafanya mazingaombwe yake halafu anaonyesha mbinu...

Mikono Yangu

Mikono inayoonekana niliyo nayo ni miwili tu. Leo nataka nifanye mazingaombwe ya ukocha, tafadhali ambatana nami. Mikono yangu isiyoonekana inaweza ikawa mingi au michache. Ninaendelea kujipima kama kocha. Je, kuna chochote ambacho umekifanya kwa utofauti na ukaona matunda na faida ya Gari yetu ya Karakana ya Ubongo? Nitafurahi kama utanipa mrejesho sahihi. Unaweza kuutoa hapa au hata inbox. Kwa kawaida, bado mwaka ni mpya na ninaendelea kukutakia Heri ya Mwaka Mpya wa 2018. Mwaka ambao tunabadilisha malengo yetu kiutendaji yawe mazuri kutekelezwa kwa kujenga tabia stahiki. Mazingaombwe yangu ya leo ni uvumbuzi wa aina yake kwa ajili ya ku-copy na ku-paste yenye faida. Mifumo yetu, masoko yetu na ugunduzi ni vitu ambavyo inabidi kuvitengeneza. Jana nimeona Mwana-Karakana aliyejitambulisha ni Mwalimu wa Piano japo ana shahada ya ugavi na manunuzi. Nikajiuliza ni kitu gani kimemsukuma ajitambulishe wakati sijatuma siku nyingi ile meseji ya namna ya kujitambulisha. Nikafanya utafi...

Mikono Isiyoonekana!

Bado tunafurahia mwaka mpya kwa namna ya kipekee kabisa. Nikiwa Kocha ninapenda kufanya kitu kinaitwa "walk the talk." Kuna Wataalamu wanasema ili kujenga tabia ni lazima urudie rudie kufanya kitu angalau siku zisizopungua ishirini na moja (21). Ila kwa wale wenye nia na dhamira nzito inachukua masaa ishirini (20) kujitengenezea tabia fulani. Mikono isiyoonekana itatumikaje kwa siku hii ndani ya Wazo la Leo? Ukizingatia jana Nilikuuliza swali, " Je, mikono yako inatumika vizuri?" Bado ninajijengea tabia kama Kocha niweze kutumia mikono yangu inayoonekana na pia ile isiyoonnekana. Nimefurahishwa na Mwana-Karakana huyu aliyetumia mikono ya kuandika yafuatayo: "Mimi leo nina watu wawili watajiunga kwenye kundi hili" Ninaweza kusema kwamba mikono yake ni sehemu ya mikono ya Kocha wenu isiyoonekana. Je, wewe una mikono mingapi isiyoonekana? Je, inafanya kazi vizuri? Tafakari! Chukua hatua pia. Ninaamini kama umetafakari vizuri utagundua mimi kocha wa...

Mikono Yako Inatumika Vizuri?

Mikono Yako Inatumika Vizuri? Kwa mara nyingine tena, narudia kukutakia Heri ya Mwaka Mpya 2018. Mikono yangu inatumika ipasavyo kuandika Wazo la Leo. Ukizingatia ile chupa ya Shampeni sasa iko tupu. Ule Mti wa Plastic uitwao Xmas Tree kwa lugha ya wenzetu uliokuwa unawaka umeshazimwa! Sina shaka mikono yako ilitumika kikamilifu. Huu ni muda muafaka wa kutafakari miezi 12 ijayo na jinsi mikono yako itakavyotumika. Je, utatumika namna gani kusababisha angalau tone la mvua lionekane mwezi huu wa January 2018? Utachambua zile nguo ambazo huvai tena? Utazifua na kuzinyoosha ili uwapatie wahitaji? Huwa Mungu anabariki kazi za mikono yetu. Mimi Kocha wako nataka tufike mahali. Ninataka baraka za Mwenyezi Mungu zishukie Karakana ya Ubongo. Mungu akipenda Januari 2018 gari letu Karakana ya Ubongo liwe linaanza kuelekea safari ya kutekeleza malengo yake. Je, uko tayari kutumia mikono yako vizuri? Kama tulivyoona kupitia Kalenda yetu, tuna malengo matatu kama ifuatavyo: 1) Kutoa New...

Tabia Na Lengo

Tabia yetu sisi ni matunda ya vile vitu vidogo vidogo tunavyofanya kila siku. Ufanisi tulio nao siyo chochote zaidi ya tabia zetu. Mafanikio hayaji kwa siku moja bali ni tabia zetu ndo zinatuvusha kutoka eneo moja A kuelekea eneo lingine B. Katika maisha yetu ya kila siku tunaweza kupata changamoto katika kujenga tabia zetu kwa sababu ya vikwazo na visingizio mbali mbali. Jinsi ya kuondoa vikwazo na visingizio hivyo ni lazima kuangalia nidhamu zetu, motisha tulizo nazo na pia jinsi tunavyojijengea malengo na tabia zetu. Unapojiwekea malengo unakuwa unachukua hatua nzito na ya maana katika kupangilia maisha yako. Kupangilia kwa kuandika malengo na utekelezaji wa malengo ni vitu ni tofauti. Kujijengea tabia fulani ni hatua muhimu zaidi ya kukusaidia kusonga mbele. Kwa mfano nina lengo la kusoma vitabu kumi mwaka 2018. Hilo ni lengo zuri. Mfano wa pili ni kujifunza tabia ya kusoma kurasa kumi au zaidi kila siku. Hiyo ni tabia. Ukilinganisha malengo na tabia ya hii mifano yetu uta...

Fanya Kazi Ya Daraja La Kwanza (Do A First Class Job)

Fanya Kazi Ya Daraja La Kwanza (Do A First Class Job) Sasa natambua ya kwamba una kila kitu kikupasacho kushinda na unashinda na sikuzote utakuwa mshindi. ONYO: Kamwe usikubali hukumu za watu wa kawaida kwani wewe si mtu wa kawaida. Kumbuka: 1. Kujiweka katika nafasi ya watu muhimu inakusaidia kufikiri vitu muhimu 2. Fikiri ya kuwa kazi yako ni ya muhimu 3. Jikumbushe kila unapopata fursa ya kufanya hivyo ya kwamba wewe ni mtu wa daraja la kwanza. 4. Katika nyakati zozote za kimaisha , jiulize ‘Hivi ndivyo mtu muhimu anavyofikiri’ Kisha heshimu jibu utakalolipata. U matokeo ya mazingira yako. Fanya kuwa sheria juu ya kutafuta ushauri kutoka kwa watu wanaojua kukuzidi. Hii itakusaidia sana kubaki daraja la kwanza. Watu hukupima kwa kuangalia ubora. Fanyia mazoezi kuwa mtu wa viwango kwa kila ufanyacho kigezo kibaki ubora wa hali ya juu mpaka ifike mahali iwe sehemu ya maisha yako na kila mtu akikuona aseme huyu ni mtu wa viwango. Acha kabisa kukubaliana na vitu chini ya viwan...

Mikakati 6 Muhimu Ili Kujijengea Kujiamini

1. Kila siku ni vyema kujikumbusha ya kwamba ulishafanya mambo mazuri siku za nyuma. Hebu tafakari yote mazuri ambayo uliweza fanikisha kuyatimiliza. a. Kikubwa mawazo yako, nguvu zako na muda wako vyote elekeza katika yale uliyokwisha wahi kuyafanikisha. HILI SI JAMBO LA KUPUUZIA HATA KIDOGO. Nashauri kufuata yafuatayo:- • Kuwa na mpango kazi wa siku. Weka vipaumbele yaani mambo yote yenye muhimu kuliko mengine ndiyo uanze nayo. Mfano unapopangilia kukutana na watu, kupitia miradi, na mengine mengi tu unayokusudia kuyatenda ni vyema kuyapanga kwa kuzingatia uzito wa kila jambo. Kikubwa mipango ya siku inayofuata ifanyike usiku kabla ya kulala. • Kuchukua Hatua/Kutenda/Kufanyia kazi mipango mkakati – Tumia muda wako vizuri kwa kuanza na mambo yote muhimu maana utakuwa umeonesha katika mpango kazi wako. Inashauriwa uwe unashughurikia malengo ya siku 60 kila mara. Nini maana yake? Kikubwa mipango yako isitoke nje katika kufikia malengo ya siku 60 na hapa ni lazima ujilazimishe kuf...

Nidhamu

Nidhamu ni kutenda kile ulichoahidi utakitenda. Hivyo nidhamu si adhabu bali ni mafunzo na ni kwa wale tuu wenye kutekeleza bila kujali hali ikoje ndio wenye kufanikisha. Kitu kimoja kinachowatenganisha waliofanikiwa na wasio fanikiwa ni kwamba; Waliofanikiwa wanatambua umuhimu wa kuwa na nidhamu na siyo kwa siku moja tu bali kwa muendelezo iwe ni kwa kujisikia au kutojisikia ni lazima kitendo husika kifanyike. Mwanadamu kwa asili ni mvivu. Na kielelezo kikubwa ni ile kauli isemayo SIJISIKII. Ndugu yangu mpendwa naomba nikupe ushauri wa bure – Mafanikio ni vita. Mapambano ni lazima. Sijawahi ona mtu aliye kwenye mapambano asipate maumivu au kujeruhiwa na hata kupoteza maisha wakati mwingine lakini hajilazi chini ati hajisikii kuendelea na mapambano. Mapambano yanaendelea mpaka ushindi upatikane na kikubwa ni kwamba mauvivu, majeraha na hata vifo kwa baadhi ya wapiganaji hutoa mafunzo ya nini kifanyike ili yaliyotokea yasijitokeze tena. Ndio maana nasema nidhamu ni mafunzo tosha. ...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...