Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 33 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza umuhimu wa mizania katika mafanikio. Tumejifunza mengi kuhusiana na masuala ya fedha na sasa ni muhimu tukajua umuhimu wa mizania katika mafanikio. Kikubwa ninachotaka kukufahamisha leo ni kuwa mafanikio sahihi ni lazima yawe yametokana na uwekezaji wa kiroho na uwekezaji halisia unaoweza onekana kwa macho ya nyama. Ni ujinga kujikita kwenye mambo ya kiroho 100% ikiwa ni pamoja na utoaji wa fungu la kumi kwa uaminifu ati kwa kuwa imeandikwa utabarikiwa kwa kuwa mwaminifu na kubaki umekaa na kusubiria baraka zimwagike. UTASUBIRI SANA na ndipo utaanza kujiuliza na kuona kama Mungu amekuacha. Hivi unawezaje mfano kuwa mwaminifu wa fungu la kumi na kushindwa kuwa mwaminifu wa kuwekeza 10% kwa uaminifu kama ilivyo kwa fungu la kumi na ukafuata kanuni zote za kufanikisha, na uone kama...