Duniani tunajifunza kila siku. Na ukikata shauri kujifunza kila siku na kufanyia kazi yale yote unayojifunza maisha yako yatakuwa yakibadilika siku baada ya siku. Unahitaji maamuzi magumu ili kubadilika. Kama kuna jambo mojawapo muhimu unatakiwa kulijua kwa kina basi ni ile saa yako ya kwanza unapokua umeachia kitanda namaanisha asubuhi uamkapo na pia saa yako moja kabla ya kulala. Ukiamka unakimbilia kufanya nini? Utafiti umeonesha ya kwamba wengi tumeathirika na jambo moja kukimbilia simu na kuanza kuangalia watsapp, face book, twitter, Instagram. Tunahitaji kubadili kwani si tabia njema. Saa moja ya kwanza baada ya kuamka kitandani ni ya muhimu sana kujua unaanza na kitu gani cha kwanza ila isiwe simu. Hapa ningefurahi kama kila mmoja angeliniambia akiamka tu anakimbilia kufanya nini? Najua itanichukua muda kupata mawazo mbalimbali lakini naamini kila mmoja anajua anachokimbilia mara aamkapo. Hakuna kanuni ya kipi uanze nacho lakini kutokana na umuhimu wa saa moja ya kwanza ku...