Habari ya leo mpendwa msomaji wa Makala zangu za kila siku sijulikanazo kwa jina la Wazo La Leo. Ni kawaida kusikia watu wakilalamika ya kuwa wanapenda sana kufanya biashara lakini tatizo hawana mtaji kuwawezesha kuanza biashara. Yawezekana hata wewe usomaye hii makala ni mmojawapo. Hili limewafanya walio wengi washindwe kuona mtaji wa kwanza ambao kila binadamu amezaliwa nao. Ikumbukwe na kuamini ya kuwa mwenyezi Mungu katika uumbaji wake alihakikisha kila binaadamu aliyemuumba alimkabidhi mtaji wa kuendesha maisha yake pasi shida yoyote. Mtaji ninaoongelea hapa ni AKILI. Akili ni kila kila kitu linapokuja suala la mchakato wa kutatua matatizo (changamoto). Shida kubwa kwa tulio wengi huwa hatutengi muda wa kufikiri na mbaya kuliko vyote hatuna tabia ya kukaa eneo tulivu ambalo ni muafaka kwa zoezi la kufikiri. Kuna nyakati akili zetu hutupa mawazo (Ideas) nzuri sana kutekeleza na kufanikisha kile tumekuwa tunakitafuta kwa muda mrefu lakini kwa kujua au kutokujua mawazo haya huja ...